Leo ZIFF tunalia, katuondoka Jasiri. Alikuwa jasiri wa mawazo na udiriki, Msema kweli asiyeogopa kuchukiwa, Mwoga wa aibu ya ukimya wa woga.

Alikuwa kijinga cha moto kiwashao msitu, Mparamia mnazi si kwa mnazi ila nazi, Mpishi wa chakula cha wanaharakati, Akashika tama kwa kuona aibu ya mvivu. .

Tama leo twalishika, katutoka wetu Leila, Hatuimbi tunalia, wimbowe hausikia, Twamsihi Maulana, amshushie dhambize, Ulale pema Jasiri, Leila bint wa Sheikh.

Martin Mhando (ZIFF)